Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea nafasi za masomo ya muda mrefu katika fani ya Sayansi kutoka Serikali ya Misri.
Masomo hayo ambayo ni kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu yatatolewa kwenye Chuo Kikuu cha Alexandria kilichopo nchini Misri chini ya udhamini wa Mpango wa Bonde la Mto Nile (Nile Basin Initiative).
Mwisho wa kuomba nafasi hizo ni tarehe 30 Mei 2019. Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi hizo na namna ya kuomba, tafadhali tembelea tovuti ifuatayo: www.nbs.alexu.edu.eg
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
10 Mei 2019
Social Plugin