Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MTANDAO WA REDIO ZA JAMII TANZANIA (TADIO) WATOA MAFUNZO KWA WARATIBU WA VIPINDI


Mtandao wa redio za jamii Tanzania- TADIO,kwa kufadhiliwa na Best Dialogue wametoa mafunzo ya siku mbili kwa waratibu wa vipindi juu ya namna ya kubuni, kuandaa na kutangaza vipindi vyenye ubora. 

Mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa ofisi za radio Dodoma fm jijini Dodoma.

Akifungua rasmi mafunzo hayo Mwenyekiti wa TADIO nchini Prosper Laurent Kwigize amesema redio za kijamii zimefanya vizuri katika tafiti zilizotolewa hivi karibu Katika uandaaji wa vipindi vinavyolenga mahitaji ya wasikilizaji lakini bado zinakabiliwa na mapungufu mbalimbali. 

Amesema TADIO kwa kufadhiliwa na Best Dialogue wameamua kutoa mafunzo hayo kwa waratibu wa vipindi ili wakafanye mabadiliko katika redio zao na kuongeza kuwa ikiwezekana katika tuzo za EJAT mwaka kesho redio hizo zitoe washindi.

Kwigize amesema pamoja na umuhimu wa waratibu wa vipindi Katika redio lakini walisahaulika badala yake mafunzo mengi yalielekezwa kwa wahariri wa vituo na kusahau kuwa waratibu ndiyo "Moyo" wa kituo cha redio. 

Naye mkufunzi wa mafunzo hayo Dotto Bulendu ambae pia ni mkufunzi chuo kikuu cha ST AUGUSTINE jijini Mwanza amewataka waratibu wa vipindi kubuni na Kuandaa vipindi vinavyoendana na Maeneo yao na yanayoweza kuwafanya wakazi wa Maeneo hayo kujimudu kiuchumi.

Mafunzo hayo yamehusisha waratibu wa vipindi wapatao 18 kutoka redio mbalimbali za Tanzania bara na visiwani na yanafanyika ikiwa radio nyingi za kijamii zinakabiliwa na chamgamoto kubwa ya ukata wa kifedha jambo ambalo linaelezwa kuwa linaweza kumalizika kwa maandalizi bora ya vipindi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com