Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Imeelezwa kuwa utafiti unaonesha kuwa takribani zaidi ya watu milioni 18 kila mwaka hufa kutokana na matatizo ya magonjwa ya moyo na wengi wao takribani asilimia 80% wanatoka katika nchi zinazo endelea ambazo zinauchumi wa kati na nchi zenye uchumi wa chini kama Tanzania.
Hayo yamesemwa na Daktari Robart Mvungi ambaye ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo na Rais wa chama cha Madktari bingwa wa magonjwa ya moyo hapa nchini katika maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la Damu Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Mei 17 ya kila mwaka ,huku akisema kuwa kati ya hivyo vifo milioni 18 theluthi moja ya vifo hivyo vinasababishwa na shinikizo la Damu.
Aidha, ameongeza kuwa utafiti unaonesha kuwa Tanzania tatizo hilo ni kubwa kwani takribani asilimia 20% mpaka 25% ya watanzania wenye umri zaidi ya miaka 24 wana shinikizo la damu iwe vijijini ama mjini.
Katika hatua nyingine ameongeza kuwa ugonjwa huo hauna dalili kwani zaidi ya asilimia 50% ya watu wote duniani walio na matatizo ya shinikizo la damu huwa hawajui na hakuna dalili maalumu , mara nyingi watu wengi wanao pata matatizo ni wale walio athirika kama ukipata kisurikari, kiharusi,shinikizo la moyo au figo ikiacha kufanya kazi vizuri.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma Dkt Wildfredius Rutahoile amesema shiniko kubwa la damu ni miongoni mwa matatizo ya moyo ambayo yanapelekea kuleta madhara makubwa sana katika afya moyo.
Sambamba na hayo rutahoile amesema kuwa kwa kawaida shinikizo la damu huwa linaanza kujengeka kidogo kidogo na linaweza kuchukua muda mrefu takribani zaidi ya miaka 10 kabla ya mtu hajaanza kupata madhara.
Hatahivyo, Dkt mvungi amesema shiniko la damu linatokana na presha kuwa zadi ya 140 ile ya juu na chini kuwa zaidi ya 90 hivyo, amewaomba watanzania kujitokeza kupima afya zao , kwani ugongwa huo hauna dalilili huku akisema kuwa zaidi ya asilimia 50% watu wote duniani walio na matatizo ya shinikizo la damu huwa hawajui.