Mpenzi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch amesema kuwa, ilibaki kidogo apate uchizi baada ya kutoka na msanii huyo.
Akizungumza na Citizen TV katika Kipindi cha 10 Over 10, Tanasha ambaye pia ni msanii wa muziki na Mtangazaji wa Radio NRG ya nchini humo alisema kuwa alipoanza kuwa na uhusiano na Diamond yalizuka maneno mabaya kwake ambayo yalitaka kumpa uchizi.
“Mwanzoni maneno hayo nilichukulia kawaida tu. Yakaanza kunifanya kupata msongo wa mawazo, lakini nilikabiliana nayo,” alisema Tanasha.
Social Plugin