Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAASISI YA UTAFITI WA WANYAMAPORI(TAWIRI ) NA FRIEDKIN CONSERVATION FUND LIMITED(FCFL) WAFUNGA VIFAA MAALUMU TEMBO 18


Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala(wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka ,Mkuu wa wilaya ya Meatu,Dk Joseph Chilongani(kulia) na Meneja wa shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL),Nana Grosse alipowasili kwenye uwanja mdogo wa ndege wa Mwiba Wildlife Ranch kushuhudia uwekaji mikanda maalumu ya ufatiliaji mienendo ya Tembo eneo la Maswa Game Reserve.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala akizungumza kabla ya kushudia uwekaji wa mikanda maalumu ya ufatiliaji mienendo ya Tembo kwenye Pori la Maswa Game Reserve uliofadhiliwa na shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) katika eneo la Mwiba Wildlife Ranch.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala(kulia) akishuhudia uweka uwekaji wa mikanda maalumu ya ufatiliaji mienendo ya Tembo kwenye Pori la Maswa Game Reserve uliofadhiliwa na shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) katika eneo la Mwiba Wildlife Ranch . 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri),Dk Janemary Ntalwila akionesha mchoro wa namna kifaa maalumu cha ufatiliaji mienendo ya Tembo kwenye Pori la Maswa Game Reserve uliofadhiliwa na shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) katika eneo la Mwiba Wildlife Ranch . 
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri),Dk Edward Kohi akizungumza mienendo na tabia za Tembo huku Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala akimsikiliza kwa makini. 
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala akifurahia jambo baada ya zoezi la uwekaji kifaa hicho kukamilika,jumla ya Tembo 18 wamewekewa mikanda yenye vifaa maalumu ya kuwafuatilia mienendo yao. 
Wataalamu wakimfuatilia mmoja wa Tembo ambaye alifungwa kifaa maalumu 
Wataalamu wa Wanyamapori wakimfuatilia mmoja wa Tembo aliyefungwa kifaa hicho kinachowawezesha kufahamu mienendo yake katika ikolojia ya uhifadhi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com