Na.Faustine Gimu Galafoni ,Dodoma.
Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imesema itaendelea kukagua na kudhibiti bidhaa za vipodozi na bidhaa nyingine na kuhakikisha bidhaa ambazo zinamfikia mwananchi zinakuwa zenye ubora ,salama na fanisi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kaimu meneja wa TFDA kanda ya kati inayo simamia mikoa ya Dodoma,singida pamoja na morogoro na Halmashauri zake zote Benedict Blush amesema TFDA imepewa jukukumu la kuthibiti,ubora,usalama pamoja na ufanisi wa bidhaa za chakula dawa,vipodozi,vifaa tiba pamoja na vitendanishi.
Aidha amesema mamlaka hiyo inafanya kazi kwa mujibu wa sheria ya chakula na dawa No 1 sura ya 219 huku akizungumzia mifumo ya udhibiti ambayo mamlaka ya chakula na dawa imekuwa ikitumia katika bidhaa za vipodozi na bidhaa nyingine.
Mbali na hilo pia amezungumzia vipodozi vyenye viambato vya sumu kama zebaki hii imekuwa na tabia ya kupenya kwenye ngozi na kadri inavyo endelea kurundikana katika mwili kunaweza kuleta shida ya ini.
Katika hatua nyingine amesema kwa wale ambao wamekuwa wakitumia viambato hivyo inaweza kusababisha kansa ya damu na hatimae kupelekea kupoteza maisha huku akigusia kwa upande wa wakina mama wajawazito ambao wamekuwa na tabia ya kutumia vipodozi kipindi cha ujazito.
Hata hivyo, amesema kama serikali inaendelea kuweka mkazo katika uthibiti wa vipodozi ili kuondoa madhara kama ambayo yanaweza kuajitokeza.