Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TFF KUPIGA MARUFUKU MATAMASHA YA MUZIKI KWENYE VIWANJA VYA SOKA...KARIA AMWAGA PESA ZA UKARABATI

Na Bakari Chijumba, Mtwara.

Shirikisho la soka Tanzania(TFF),limetenga jumla ya Dollar za kimarekani Million moja,kwa ajili ya kurekebisha viwanja kumi vya soka nchini,ikiwemo uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo mjini Mtwara.

Akizungumza na wanahabari Mkoani Mtwara,06 Mei 2019,Rais wa TFF Wallace Karia,amesema kati ya viwanja hivyo kumi, kila uwanja umetengewa Dollar laki moja.

"Kwenye mkutano mkuu uliofanyika Arusha,tulipeleka maombi kwa wajumbe,Kutenga Dollar Million moja ili kurekebisha viwanja kumi,ikiwemo hiki cha Nangwanda(Mtwara)..Tunaboresha Pitch(Dimba),vyumba vya Waamuzi na vyumba vya  kubadilishia wachezaji,pia eneo la wanahabari" amesema Karia.

Aidha Karia amesema katika kuhakikisha ubora wa viwanja hivyo kumi unaendelea kuimarishwa, wameanza mazungumzo na wamiliki wa viwanja hivyo(CCM),ili TFF ibebe jukumu la kusimamia mazingira ya ndani ya viwanja pindi ukarabati utakapokamilika.

"Tupo kwenye mazungumzo na wamiliki wa viwanja hivi kumi,vyote vinamilikiwa na CCM,ili tutakapovirekebisha eneo la katikati ya uwanja libaki kwa ajili ya mpira tu na siyo shughuli za muziki au  maonesho mengine, labda iwe shughuli za kitaifa..Hatutoruhusu kabisa shughuli tofauti na mpira na tutaomba CCM wabaki na maduka yanayozunguka uwanja,usimamizi wa Dimba watuachie sisi tutajua tunagawana vipi upande wa mapato" amesema Karia na kuongeza kwamba;

"Nasisitiza tukishavirekebisha viwanja hivyo,hatutoruhusu kutumiwa tofauti na shughuli za kisoka, bahati nzuri katibu wa Ccm tumekutana nae na wiki ijayo tunakwenda kukaa  nae ..kuhusu hela zipo, katika  hela ya FIFA Doola Milion 5 tumetenga  Dola million moja kwa kila kiwanja Dola laki moja"

Katika hatua nyingine Karia ametoa wito kwa viongozi kutoka kwenye maeneo ambayo viwanja hivyo vinakarabatiwa,kuweka jitihada za dhati ili kufanikisha hatua nyingine zitakazosalia.

"Rai yangu kwa vjongozi wa serikali, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wanachi wa mikoa tutakayotengenza viwanja, fedha ni kidogo ni  kidoog tunataka kurekebisha pia na sehemu ya wageni maalumu kupumzika (High Table), wadau watapatie Materials(Vitendea kazi) na sisi tutagharamia ufundi...Nyasi hazitokuwa za bandia ni za kawaida,tutatengeneza  miundombinu ya visima vya kumwagilia nyasi hizo...Ligi ikiisha tu tutaanzaa marekebisho hayo" amesema Karia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara(MTWAREFA),Athmani Kambi ameishukuru TFF kwa uamuzi huo na kusema watashirikiana nao katika kuhakikisha uwanja wa Nangwanda unakuwa bora na wa kisasa.

"Naishukuru TFF ya sasa,nimekaa na TFF miaka kumi na kitu ila sijawahi kuona TFF ambayo inaweza kutoa Dola laki moja kukarabati viwanja..Pia tuwashukuru kwakuwa kwenye viwanja kumi na Nangwanda tumepewa fursa" amesema Athmani Kambi na kuongeza kuwa;

"TFF imetoa Dollar Laki moja,itatengeneza pitch,vyumba vya kubadilishia na eneo la wanahabari(Nangwanda)..Tutaongea na Mkuu wa Mkoa tupate wadau wengine watusaidie kujenga Majukwaa,Ndanda Sc ikifanya vzuri kama sasa hivi watu wanajaa ila majukwaa hayatoshi, tutapambana kukamilisha uwanja .


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com