Rais wa Marekani Donald Trump alizungumza kwa njia ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin hapo jana kuhusu suala la nyuklia, uwezekano wa kuishawishi China kusaini mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia, pamoja na mgogoro wa Venezuea ambako Urusi inaunga mkono upande wa serikali na Marekani inaunga mkono upinzani.
Msemaji wa ikulu ya Marekani Sarah Sanders amesema katika mazungumzo hayo ya zaidi ya saa nzima, viongozi hao wawili pia walijadili suala la Ukraine, Korea Kaskazini, na biashara kati ya Urusi na Marekani.
Baada ya mkutano, Trump aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba alikuwa na mazungumzo marefu na rais wa Urusi na kwamba kuwa na uhusiano mzuri na Urusi pamoja na China ni jambo zuri kwa Marekani.
Social Plugin