Mbunge Tundu Lissu amesema atarejea nchini Septemba 7, 2019, siku ambayo itatimia miaka miwili tangu aliposhambuliwa kwa risasi jijini Dodoma Septemba 7, 2017, Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji kwa matibabu alishambuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Mara baada ya kushambulia, mwanasiasa huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na usiku wa siku hiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikopata matibabu hadi Januari 6, 2018 na kuhamishiwa Ubelgiji kuendelea na matibabu zaidi.
Lissu ambaye kwa sasa anatembea kwa msaada wa gongo moja akizungumza na wapiga kura wake mwishoni mwa wiki kupitia simu ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema anarudi nchini Septemba 7, 2019.
Amesema katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Oktoba, 2019 atakuwepo Tanzania.