UFAHAMU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE

Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi viitavyo Dengue vinavyosambazwa na mbu aina ya Aedes.
 

Mbu huyu anayeambukiza homa ya dengue hupendelea kuishi karibu na makazi ya watu na huweza kuuma binadamu mchana na usiku. 

Ugonjwa huu huathiri sana nchi za tropiko kama Amerika ya kusini na Africa. Ni moja kati ya homa kali inayodhoofisha na  kuambatana na maumivu makali. 

Kwa sasa, hakuna kinga ya homa ya dengue, njia pekee ya kuepuka ugonjwa huu ni kuzuia kuumwa na mbu anayesambaza homa ya dengue.
Dalili za homa ya dengue

•Homa kali ya ghafla

•Maumivu makali ya kichwa

•Macho kuuma

•Maumivu ya viungo

•Kichefuchefu

•Kutapika

•Vipele ambavyo hutokea siku nne baada ya homa kuanza

•Kutoka damu puani, kwenye fizi na kuchubuka kirahisi

Mara nyingi dalili huwa sio kali na wengi hudhania ni homa ya mafua au maambikizi mengine ya virusi. Dalili hizi huanza kutokea baada ya wiki mbili, lakini kwa wengi huchukua wiki moja ya kwanza na tayari utaanza kuona dalili za dengue.

Matatizo ambayo yanaweza kutokea baada ya maambukizi ya homa hii ni

•Homa kali zaidi

•Kuharibiwa kwa tezi na mishipa ya damu

•Kutokwa na damu zaidi puani na kwenye fizi

•Ini kuwa kubwa

•Na huweza kupelekea kifo

Vipimo

•Damu huchukuliwa na kuangalia virusi vya dengue au

• Kingamwili dhidi ya virusi hizi

Matibabu

Mpaka sasa hamna dawa kwa ajili ya ugonjwa huu ila  dawa za kupunguza homa na maumivu huweza kutumika kwa mfano:

•Paracetamol

•Pumzika vya kutosha

•Kunywa maji

•Nenda hospitali ukapate ushauri wa daktari



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post