Hali iliyotarajiwa kuwa ya furaha na mahaba tele kati ya wapenzi wawili huko Funyuka, Kaunti ya Busia nchini Kenya imegeuka na kuwa karaha baada ya mwanamke kumuuma mwenzake ulimi.
Michael Otieno ambaye ni bawabu alinyemelea na kuingia katika nyumba ya Philister Akinyi Jumapili, Mei 5,2019 na hapo ndipo alipokutana na masaibu yake.
Wapenzi wakipigana busu la ndimi. Mpango wa Kando'mchepuko' amemuuma mwenzake ulimi huko Busia.
Inadaiwa na walioshuhudia kuwa, Otieno alikimbizwa hospitalini na majirani waliofika kumsaidia akilia kwa uchungu mwingi.
Kulingana na naibu chifu wa Namuduru Josephat Sundya, wawili hao wamekuwa wapenzi kwa karibia miaka mitano sasa tangu kifo cha mume wa Akinyi.
Katika siku za karibuni, mahaba kati ya wawili hao yamekuwa yakishuhudia migogoro ya mara kwa mara na inadaiwa bawabu huyo, 50, ameamua kuachana na mpenzi wake na kumrudia kikamilifu mke wake halali.
Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Busia alikokuwa amekimbizwa na majirani kupewa matibabu, Otieno alikana madai eti walikuwa wakifanya ngono wakati kisa hicho kilipotokea.
Alimshutumu mwanamke huyo kwa kumshambulia alipomwomba asimdhuru mke wake halali.
Chanzo- Tuko
Social Plugin