Ibrahim Ismail, jamaa mwenye umri wa miaka 20 amepatikana na hatia ya kula embe wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na kupokea mijeledi 40 kwa kosa hilo.
Ismail ambaye alituhumiwa kula wakati Waislamu wengine wakifunga, amepatikana na hatia hiyo na mahakama inayoongozwa na sheria za Shariah katika eneo la Ringim, mjini Jigawa, nchini Nigeria.
Ibrahim Ismail alipokea mijeledi 40 kwa kula embe wakati wa mfungo wa Ramadhan katika soko la Ringim baada ya afisa wa mahakama kumsomea mashtaka
Jaji Safiyanu Ya’u, alitoa amri kwamba jamaa huyo acharazwe mijeledi 40 hadharani ili iwe funzo kwake na kwa wengine ambao walikaidi sheria za mwezi mtukufu.
Kushiriki mlo kwa wakati usiofaa inakinzana na sheria za kifungu cha 370 za mji wa Jigawa, Nigeria.
Awali, Nabahani Usman ambaye ni kamanda wa polisi wa Kano Hisbah, alionya kwamba yeyote atakayepatikana akila ovyo ovyo hadharani atachukuliwa hatua kali kwa kukaidi sheria za mfungo wa Ramadhan.
Aliongeza kuwa, wale watakaonaswa wataachiliwa huru iwapo watatoa ushahidi wa ripoti ya daktari kwamba walikuwa wanaruhusiwa kula kwa sababu za kiafya.
Chanzo - Tuko