Waasi wa Kihouthi nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran wamesema leo kuwa wameushambulia uwanja wa ndege katika mji wa mpaka wa Saudi Arabia kwa mara ya pili mfululizo wakati mivutano ya kikanda ikiendelea.
Saudia, mshirika wa kikanda wa Iran, inaongoza kampeni ya kijeshi nchini Yemen dhidi ya Wahouthi.
Televisheni inayoegemea upande wa Wahouthi ya al-Masirah imeripoti kuwa shambulizi hilo la ndege isiyoruka na rubani ilizilenga barabara za uwanja wa ndege wa mji wa kusini magharibi mwa Saudia wa Najran.
Televisheni hiyo, ikinukuu duru ya jeshi la Houthi, imesema shambulizi hilo lilifanikiwa, bila ya kutoa maelezo zaidi.
Hapo jana, wahouthi walisema waliushambulia uwanja wa ndege wa Najran na kulenga ghala la silaha.
Mashambulizi hayo yaliyothibitishwa na Saudia, yanakuja wakati mivutano ikiendelea kati ya Marekani, mshirika wa Saudia, na Iran.
Social Plugin