Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akizungumza na baraza la madiwani wa Kondoa kabla ya kuanza ziara ya kuwasha umeme katika kijiji cha Mauno pamoja kituo cha Afya cha Busi mkoani Dodoma.
Sehemu ya madiwani wakimsikiliza Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika kikao hicho
Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akizungumza na wananchi wa Kinyasi alipfanya ziara ya kuwasha umeme kijiji cha Mauno pamoja na Kituo cha Afya cha Busi wilayani Kondoa
Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akiwaonyseha wananchi kifaa cha kuunganishia umeme
Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani akiwakabidhi wananchi kifaa cha kuunganishiwa umeme katika kitongoji cha Kinyasi.
Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akimueleza jambo mbunge wa Kondoa ambaye pia ni Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kabla ya kuwasha umeme katika kituo cha Afya cha Busi
Waziri wa Nishati,Dk.Merdard Kalemani,akisisitiza jambo kwa wananchi wa kijiji cha Busi kabla ya kuwasha umeme katika kituo cha Afya
Baadhi ya wananchi wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nishati,Dk.Merdard Kalemani alipokuwa anazungumza nao kabla ya kuwawashia umeme katika kituo cha Afya cha Busi.
Waziri wa Nishati,Dk.Merdard Kalemani,akiwasha umeme katika kituo cha Afya cha Busi wilaya ya Kondoa.
Picha Zote na Alex Sonna-Fullshangwe blog
***
WAZIRI wa Nishati Dk. Medard Kalemani amewataka wakazi wa vijiji vya Mauno na Busi wilayani Kondoa ambao bado hawajajenga kwenye maeneo yao kuweke miti ili wasogezewe huduma ya umeme kwa haraka.
Pamoja na hayo, amemwagiza Meneja wa shirika la umeme (Tanesco) pamoja na mkandarasi kuhakikisha wanamaliza kusambaza huduma ya umeme katika vijiji vyote vilivyosalia wilayani Kondoa ndani ya wiki moja.
Waziri Kalemani ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Mauno pamoja na kituo cha Afya cha Busi huku akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Kondoa ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
Waziri Kalemani amewataka wananchi hao kuwa, kuanzia sasa uunganishwaji wa umeme ni sh. 27,000 tu, uwe wa Tanesco au Rea huku akiahidi kupiga mnada wa kuku wa mkazi ambaye atashindwa kulipia kiasi hicho kwa ajili ya kuunganishiwa huduma hiyo.
Kalemani amefafanua kuwa Tanesco kupitia mkandarasi hawana sababu ya kusuasua kuwasha umeme katika maeneo hayo kwa kuwa nguzo na nyaya wanazo za kutosha.
Aidha Waziri Kalemani ameahidi kurejea kwenye kata hiyo mwezi ujao kufuatilia agizo lake.
Mbunge wa Kondoa,Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji,aliwataka wananchi kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali za kuwapelekea huduma ya umeme kwa kutumia fursa hiyo kuingiza umeme katika nyumba zao.
Pia ameishukuru Serikali ya awamu ya Tano kwa jitihada kubwa inazozifanya kupeleka maendeleo kwa wananchi na kujali wananchi wanyonge na wenye hali ya chini.
Mmoja wa wakazi kijijini cha Busi Bw.Nuru Bi Mdanga akizungumza baada ya kuwashiwa umeme ameelezea furaha yake ya kupunguzwa kwa gharama ya uunganishwaji wa huduma hiyo pasipokujali unatokea Rea au Tanesco.
Social Plugin