Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda, amewashauri Watanzania kula korosho kwa sababu zina virutubisho vya kurudisha heshima ndani ya ndoa.
Kakunda ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Mei 16, kuwaelezea maendeleo ya ununuzi wa korosho, ambapo pamoja na mambo mengine amesema hata watu wa mikoa ya kusini wanazaliana sana kwa sababu wanakula korosho kwa wingi.
“Korosho ni kirutubisho kizuri, ni ajabu Watanzania hawataki kuzitumia, zinaongeza virutubisho, na kuongeza heshima ya ndoa.” amesema Waziri Kakunda.
Social Plugin