Na Amiri kilagalila
Waziri wa Nishati Dkt.Medad Kalemani amewataka wananchi kutunza miundombinu ya Umeme inayopita katika vijiji vyao.
Akizungumza katika Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Masasi Jana,waziri kalemani amesema kuwa serikali inatumia gharama kubwa kufikisha umeme na kuwataka wananchi wasifanye shughuli zitakazo athiri miundombinu ya Umeme ikiwemo kuwasha moto karibu na Nguzo na badala yake wahamasike kulipia huduma ya Umeme ili iweze kuwasaidia katika shughuli zao za kiuchumi
Akiwasha umeme katika vijiji vya Nanditi na Mombaka katika Wilaya ya Masasi Waziri amezitaka halmashauri za wilaya, kulipia gharama za Umeme za taasisi mbalimbali za kijamii ikiwemo Shule na zahanati na kudai umeme mara tu baada ya kulipia.
“Kabla ya kulalamika shule haina umeme na zahanati haina umeme, jiulize swali moja tu umelipia?lipia kwanza ndo udai umeme, halmashaur zote za wilaya lipieni taasisi za umma, tunataka wananchi wapate umeme, na umeme pia ufike mashuleni, zahanati, na sehemu zote zinazotoa huduma” alisema Dkt.Kalemani na kumtaka Mkandarasi kukamilisha kuunganisha umeme katika vijiji 122vilivyobaki katika kata ya Mndibwa, ndani ya siku 25.
Naye Mkuu wa wilaya ya Masasi,Mhe. Selemani Mzee ameiashukuru Serikali kwa kufikisha Umeme Masasi na kuwataka wananchi wote wa masasi kulipia Umeme.
Social Plugin