WAZIRI KALEMANI AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MIUNDO MBINU YA UMEME

Na Amiri kilagalila
Waziri wa Nishati Dkt.Medad Kalemani amewataka wananchi kutunza miundombinu ya Umeme inayopita katika vijiji vyao.


Akizungumza katika Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Masasi Jana,waziri kalemani amesema kuwa serikali inatumia  gharama kubwa kufikisha umeme na kuwataka wananchi wasifanye shughuli zitakazo athiri miundombinu ya Umeme ikiwemo kuwasha moto karibu na Nguzo na badala yake wahamasike kulipia huduma ya Umeme ili iweze kuwasaidia katika shughuli zao za kiuchumi

Akiwasha umeme katika vijiji vya Nanditi na Mombaka katika Wilaya ya Masasi Waziri amezitaka halmashauri za wilaya, kulipia gharama za Umeme za taasisi mbalimbali za kijamii ikiwemo Shule na zahanati na kudai umeme mara tu baada ya kulipia.

“Kabla ya kulalamika shule haina umeme na zahanati haina umeme, jiulize swali moja  tu umelipia?lipia kwanza ndo udai umeme, halmashaur zote za wilaya lipieni taasisi za umma, tunataka wananchi wapate umeme, na umeme pia ufike mashuleni, zahanati, na sehemu zote zinazotoa huduma” alisema Dkt.Kalemani  na kumtaka Mkandarasi kukamilisha  kuunganisha umeme katika vijiji 122vilivyobaki  katika kata ya Mndibwa, ndani ya siku 25.

Naye Mkuu wa wilaya ya Masasi,Mhe. Selemani Mzee ameiashukuru Serikali  kwa kufikisha Umeme Masasi na  kuwataka wananchi wote wa masasi kulipia Umeme.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم