Picha : DIWANI ZUHURA WAZIRI AENDESHA BONANZA LA MICHEZO IBADAKULI



Diwani wa viti maalumu Manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri anayetoka tarafa ya Ibadakuli ameendesha Bonanza la michezo kwenye Kata ya Ibadakuli mjini Shinyanga ili kuibua vipaji vya vijana kimchezo, pamoja kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Bonanza hilo la michezo limefanyika leo Mei Mosi 2019 kwenye viwanja vya michezo vya Bugweto, kwa kucheza mpira wa miguu, kukimbiza kuku, kuvuta kamba, kucheza drafti pamoja na mbio za baiskeli, ambapo washindi walipewa zawadi zao.

Akizungumza kwenye Bonanza hilo Diwani huyo wa Viti maalumu Zuhura Waziri, amesema lengo na madhumuni ni kuinua vipaji vya vijana, kuimarisha umoja, kudumisha amani, pamoja kumuunga mkono Rais John Magufuli ambaye amekuwa mfano wa kuigwa kusaidia kuinua michezo hapa nchini.

“Bonanza hili limeshirikisha timu nne za mpira wa miguu kutoka Uzogole, Mwagala, Ibadakuli, pamoja na Bugweto , wananchi wameshiriki kwenye michezo mbalimbali ikiwamo kukimbiza kuku, kuvuta kamba, kucheza drafti na mbio za baiskeli, ili kuwauganisha kuwa kitu kimoja na kuinua vipaji vya vijana,”amesema Waziri.

“Mbali na bonanza hili pia natarajia kuunda timu ya kata ya Ibadakuli ambayo itakuwa ikishiriki kucheza ngazi ya wilaya, ili kuendelea kuinua vipaji vya vijana kwenye kata hii, ambapo watakuja kuchezea kwenye Timu kubwa na hatimaye kupunguza tatizo la ajira, ikiwamo timu ya hapa nyumbani Stand United,” ameongeza.

Naye Mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu, amempongeza diwani huyo wa viti maalumu kwa kuanzisha bonanza hilo, ikiwa michezo kwa sasa inatoa ajira nyingi kwa vijana na kutoa wito kwa wanamichezo hao wajitume kwenye michezo hiyo, ili baadae wakacheze kwenye timu kubwa.

Pia amewatahadharisha vijana kuwa makini kuelekea  kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, wasikubali kurubuniwa na baadhi ya vyama na kuvuruga amani ya nchi, bali wawe makini pamoja na kuchagua viongozi ambao watawaongoza vyema na kuwaletea maendeleo kama inavyofanya Serikali ya CCM Chini ya Rais John Magufuli.

Kwa upande wao vijana walioshiriki michezo hiyo akiwamo Makoja Seni , wamemshukuru diwani huyo kwa kufanya Bonanza hilo la michezo ambalo limewapa moyo wa kufanya mazoezi ili kuendeleza vipaji vyao, ambavyo hapo  baadae vitakuja kuwapatia ajira na kuinuka kiuchumi.

Aidha katika Bonanza hilo,Makoja Seni aliibuka mshindi wa mbio za baiskeli, kukimbiza kuku kwa upande wa wanawake Halima Husein, huku wazee akiibuka Loyce Jiledya, Draft Samweli Kashinje, kuvuta kamba ukipata ushindi mtaa wa Mwagala kwa wanaume, wanawake mtaa wa Bugweto “A”.

Upande wa mpira wa miguu timu ya Bugweto ndiyo wameibuka washindi ambapo wamepewa seti moja ya jezi pamoja na Mpira, wakifautiwa na Timu ya pili ambayo ni Ibadakuli ambao walipata seti moja ya jezi, huku mshindi watatu akiwa ni Mwagala akifuatiwa na Uzogole ambapo wote walipewa mpira mmoja mmoja.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Diwani wa Viti maalumu manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri akizungumza kwenye Bonanza la Michezo Kata ya Ibadakuli lililofanyika kwenye eneo la Bugweto na kuelezea madhumuni kuwa ni kuinua vipaji wa vijana pamoja na kutekelezea ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abuu Hafeez Mukadamu akiwaasa vijana kujituma kwenye michezo yao ili ipate kuwasaidia kupata ajira na kuwainua kiuchumi.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini (UVCCM) Dotto Joshua, akiwataka vijana kupenda michezo ambayo pia itawasaidia kupata afya njema, kupendana pamoja na kudumisha amani ya nchi.

Diwani wa Kata ya Ibadakuli Msabila Malale akizungumza kwenye Bonanza hilo na kuwataka vijana kudumisha nidhamu kwenye michezo yao na kumpongeza diwani huyo wa viti maalumu Zuhura Waziri kwa kufanya Bonanza hilo ambalo ni muhimu kwa vijana.

Vijana wakisikiliza nasaha kutoka kwa viongozi mbalimbali kwenye Bonanza hilo la Michezo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu, akifungua Bonanza hilo la Michezo kwenye viwanja vya michezo Bugweto.

Bonanza likianza kwa mashindano ya mbio za Baiskeli.

Mbio za Baiskeli zikiendelea.

Wananchi wakishuhudia mashindano ya mbio za Baiskeli.

Mshindi wa mbio za Baiskeli Makoja Seni akiibuka na ushindi mara baada ya kuwashinda wenzake kwa kuzunguka  Round 60.

Mashindano ya kufukuza kuku yakiendelea.

Halima Husein akiibuka mshindi wa kufukuza Kuku na kisha kuondoka na kitoweo hicho.

Mzee Loyce Jiledya akiibuka mshindi wa kufukuza kuku mara baada ya kuwazidi wazee wenzake na kisha kuondoka na kuku huyo.

Mashindano ya uvutaji wa kamba ukiendelea ambapo washindi waliibuka vijana kutoka Mtaa wa Mwagala.

Mashindano ya kucheza Draft yakiendelea ambapo mshidi aliibuka Samweli Kashinje.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu.

Penat zikipigwa mara baada ya Timu ya vijana ya ufunguzi wa Bonanza hilo, kutoka Bugweto A na B kumaliza dakika 90 bila ya kufungana, ambapo mwenye Jezi ya Njano ni mchezaji kutoka Bugweto B, akipiga Penati na kupata Goli na hatimaye kupata ushindi.

Mchezo kati ya Bugweto FC wenye Jezi Nyekundu ambao ndiyo mabigwa wa Bonanza hilo , wakicheza mchezo wa kirafiki na Bugweto Veterani wenye Jezi ya Njano, ambapo Bugweto FC waliibuka na ushindi wa Goli Moja.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Aboo Hafez Mukadamu, katikati, akiwa na Diwani wa Kata ya Ibadakuli mkono wa kulia na kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua, wakiangalia mashindano mbalimbali kwenye Bonanza hilo.

Kabumbu likiendelea kusakatwa kwenye Bonanza hilo.

Mmoja wa wananchi akiwa amepanda juu ya mti kushuhudia michezo mbalimbali kwenye Bonanza hilo la michezo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa mbio za Baiskeli kwa mwenyekiti wao Kande Maganga.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa mshindi wa Draft Samweli Kashinje.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa Tatu na Wanne wa mpira wa miguu.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa Pili wa mpira wa miguu Timu ya Ibadakuli kwa kupewa Seti moja ya Jezi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafeez Mukadamu akitoa zawadi kwa washindi wa kwanza wa mpira wa miguu kutoka Timu ya Bugweto ambapo walipewa Seti moja ya jezi pamoja na Mpira.

Mfugaji Bora kwenye michezo ya mpira wa miguu kwenye Bonanza hilo Raymond Peter akipewa zawadi.

Washindi kutoka timu ya Bugweto wakipiga picha ya pamoja.
Mara baada ya kumaliza Bonanza hilo la michezo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Hafez Mukadamu akimkabidhi kadi ya uanachama ya CCM Daudi Msabila ambaye amehamia kwenye chama hicho kutoka upinzani.

Burudani zikiendelea kutawala mara baada ya Bonanza hilo la michezo likimalizika ambapo Diwani huyo wa Viti maalumu Zuhura Waziri ambaye ndiye muandaaji, akicheza wimbo na wananchi uitwao Iokote wa msanii Maua Sama

Wimbo wa msanii Maua Sama Iokote ukiendelea kutawala kwenye kufunga Bonanza hilo la michezo.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post