Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktarina watoa huduma za afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi mjini Morogoro leo Mei 6, 2019. Mafunzo hayo ambayo yamewaleta pamoja madaktari kutoka hospitali na umma na binafsi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akitoa neon la utangulizi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe (wapili kulia), akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba, mara baada ya kufungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari n a watoa huduma za afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi. Mafunzo hayo yaliypowaleta pamoja Zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa mitano imeanza leo Mei 6, 2019 mjini Morogoro. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ttahmjni wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria, WCF, Bw.Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu masuala ya kisheria katika kutekeleza majukumu ya Mfuko.
Mkurugenzi Mkuu, Bw. Mshomba (wapili kushoto), akibadilishana mawazo na wataalamu (wawezeshaji), Daktari bingwa mbobezi wa mifupa na viungo nchini, Dkt. Robert Mhina(watatu kushoto), Dkt. Hussein Mwanga na Bw. Yahya Kishashu.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, MOROGORO
MKUU wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe, amewaasa madaktari kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi kwa kuzingatia miongozo iliyopo.
Dkt. Kebwe ametoa wito huo leo Mei 6, 2019 wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari na watoa huduma za afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi mjini Morogoro.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam na Morogoro wanashiriki mafunzo hayo.
“Mnapofanya tathmini vizuri mnausaidia Mfuko kulipa fidia stahiki, mfanye tathmini kwa haki, msije mkaingia kwenye mtego msikubali kurubuniwa na huu ndio wito wangu kwenu.” Alisema.
Dkt. Kebwe aliupongeza Mfuko kwa hatua iliyofikia hususan katika eneo la kutoa elimu kwa wadau kama madaktari ambao ndio huuwezesha Mfuko kutekeleza wajibu wake wa ulipaji Fidia kwa usahihi.
“Kwa sasa tayari mmetoa mafunzo kwa madaktari 764 kote nchini na leo hii idadi nyingine inaongezeka hili ni jambo ambalo mnastahili pongezi kwa kufikia hatua hii katika muda mfupi wa uhai wa Mfuko.” Alisema Dkt. Kebwe.
Alisema Mfuko huu ni muhimu katika nchi yetu katika kipindi hiki ambacho taifa linajenga uchumi wa viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema licha ya kutoa mafunzo hayo, lakini pia Mfuko hutumia fursa hiyo kuwaelimisha kuhusu shughuli za Mfuko.
Alisema mafunzo hayo yatatolewa na wataalamu kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa kushirikiana na watalamu kutoka Taasisi ya Mifupa MOI na MUHAS.
Aidha Bw. Mshomba alimpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuona umuhimu wa kipekee katika kujenga uchumi wa viwanda kwa kuweka kipaumbele kwa nchi yetu kama namna ya kutufikisha kwenye uchumi wa kati ifikapo 2020-2025 kwani ni ukweli ulio wazi kwamba hakuna nchi iliyoendelea Duniani bila ya kuwa na uchumi wa viwanda na nilazima wote kama watanzania tusimame pamoja kumsaidia Mhe. Rais.
“Sisi kama Mfuko tutamsaidia Mhe. Rais katika azama yake kwa kuahkikisha kwamba, tunafanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha na kuwakinga wafanyakazi kwa kutoa elimu ili kuhakikisha kwamba tunalinda nguvu kazi ya taifa kwa kuzuia ajali makazini au kuzipunguza na hata zinapotokea basi malipo ya Fidia yanafanyika kwa haraka”. Alisema.
Social Plugin