Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ZITTO AIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI DHIDI YA VIJANA WANAOJIPAKA OIL CHAFU NA KUBAKA WANAWAKE


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe ameiomba Serikali kuingilia kati dhidi ya baadhi ya vijana  wanaokuwa wakijipaka Oil Chafu na kuvamia wanawake  na kuwabaka   jambo ambalo ni Udhalilishaji wa kijinsia. 


Zitto ametoa ombi hilo leo Mei 21,2019  mbungeni jijini Dodoma wakati  akiwasilisha hoja ya dharura ambapo amesema suala la baadhi ya vijana kujipaka oil chafu na kuvamia wanawake  na kuwabaka limekuwa likijitokeza mara kwa mara jimboni kwake ambapo amebainisha kuwa lengo la kujipaka Oil chafu kwa vijana hao ni kurahisisha kuteleza na  kutojulikana sura zao pindi wanapokamatwa. 


Mhe.Zitto amesema mpaka sasa kuna jumla ya Matukio 43 ya unyanyasaji wa wanawake jimboni kwake tangu Mwaka 2016  na wamekuwa wakipokea vipigo mbalimbali kutoka kwa vijana hao wahuni ,hivyo kuna haja ya serikali kuingilia kati ili kulinda usalama wa wanawake. 


Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya     ndani ya Nchi,Kangi Lugola amesema serikali ya Tanzania haiwezi kuvumilia vitendo vya kinyama na udhalilishaji kuendelea katika nchi ya Tanzania hivyo atahakikisha  vitendo hivyo vinadhibitiwa  


Hata hivyo,Waziri Lugola amesema kuna baadhi ya Taasisi zimekuwa zikifanya uchunguzi na kukuza mambo na kujenga hofu kwa wananchi hata kama ni madogo  hali na serikali imeshaanza kuziorodhesha taasisi hizo hali iliyoleta mvutano bungeni kati ya Waziri wa Mambo ya ndani na Zitto Kabwe. 


Mwenyekiti wa Bunge Mhe.Nagma Giga amesema suala la ubakaji sio la kuvumiliwa liwe dogo au kubwa hivyo amemwagiza Waziri wa Mambo ya ndani Kangi Lugola kushughulikia jambo hilo.


 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com