Aliyekuwa meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amejiunga na Miamba ya Italy Juventus ambapo amesaini kandarasi ya miaka mitatu.
Juventus, wamemtangaza Sarri kuwa meneja wao mpya, akichukua mikoba ya Massimiliano Allegri, aliyeachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita.
Sarri amedumu kwenye kikosi cha Chelsea kwa miezi 11 huko Stamford Bridge, akiwaongoza kubeba ubingwa wa Europa Ligi na kuwarudisha kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita.
Social Plugin