Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imesema ahadi ya Rais Magufuli ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya kutoka Kahama ,Bulyang’hulu hadi Geita yenye urefu wa km 120 ipo palepale na wakati wowote ujenzi unaweza kuanza.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Elias Kwandikwa amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Busanda ,Mkoani Geita Lolensia Bukwimba aliyehoji juu ya ahadi mbalimbali za serikali juu ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Kahama hadi Geita ,ni lini Serikali itaanza kutekeleza ahadi hizo.
Katika majibu yake,Naibu waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe,Elias Kwandikwa amesema ahadi ya Rais John Pombe Magufuli katika ujenzi wa Barabara mbalimbali hapa nchini ikiwemo barabara ya Kutoka Kahama,Bulyangh’ulu,Bukoli hadi Geita ipo palepale na ujenzi unaweza kuanza muda wowote kuanzia sasa.
Ikumbukwe kuwa ,taratibu za kuomba kupandishwa hadhi barabara zimeainishwa kwenye kanuni Na.43 na 44 za mwaka 2009 za sheria ya barabara Na.13 Ya mwaka 2007 ambapo bodi ya mkoa ya barabara [Regional Roads Boards] huwasilisha maombi kwa Waziri anayehusika na Barabara tajwa kama itakuwa imekidhi vigezo vya kupandishwa hadhi.
Social Plugin