Nadia Rajab enzi za uhai wake
Binti aitwaye Nadia Rajab (18) mkazi wa Kambarage Mjini Shinyanga amefariki dunia baada ya pikipiki aliyokuwa amepanda ikiendeshwa na Othuman Hassan (30) askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), mkazi wa Old Shinyanga kuacha njia na kugonga kingo ya barabara.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP,Richard Abwao ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Juni 22,2019 majira ya saa tisa na dakika 40 alfajiri katika barabara ya Uhuru, maeneo ya Total Petrol Station kata ya Shinyanga Mjini, Manispaa ya Shinyanga.
“Pikipiki yenye namba za usajili MC. 402 BYN aina ya SANLG iliyokuwa ikiendeshwa na Othman Hassan ambaye ni askari wa JWTZ, mkazi wa Old Shinyanga iliacha njia na kugonga kingo ya barabara na kusababisha kifo kwa abiria wake aliyekuwa amembeba kwenye pikipiki hiyo aitwaye Nadia Rajab”,amesema Kamanda Abwao.
Kamanda Abwao amekitaja chanzo cha tukio hilo kuwa ni uzembe wa dereva kuendesha pikipiki akiwa amelewa na tayari dereva amekamatwa na pikipiki husika ipo kituoni.
Na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Social Plugin