Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,Kangi Lugola amewataka askari kote nchini kuacha tabia ya kukamata ovyo waendesha bodaboda na kuziweka kizuizini pikipiki zao katika vituo vya polisi bila sababu na makosa ya Msingi.
Waziri Lugola amesema hayo Juni 17,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu maswali mbalimbali ya yaliyoelekezwa katika Wizara yake ambapo wamedai pamekuwepo na changamoto ya baadhi ya askari wa vikosi vya usalama barabarani kuonekana kuwa kero kwa waendesha bodaboda kutokana na kukamata pikipiki na kuziweka kizuizini kwa muda mrefu licha ya makosa hayo kuwa na uwezekano wa kutatulika kwa utaratibu maalum.
Akijibu Maswali hayo,Waziri Lugola amesema pikipiki inaweza ikakamatwa na kuwekwa kizuizini katika kituo cha polisi kwa makosa matatu ambayo ni endapo imehusika kwenye uhalifu,imeokotwa na haina mwenyewe na sababu ya tatu imesababisha ajali kinyume na hapo hairuhusiwi kukamatwa na kupelekwa kituoni.
Aidha,Waziri Lugola amesema ajali za barabarani zimekuwa zikitokea mara kwa mara hapa nchini ,hivyo watanzania wanatakiwa kufuatilia bima pindi wanapopata ajali.
Awali akijibu Swali la Msingi la Subira Mwaifunga,Mbunge wa viti Maalum,lililohoji juu ya tishio la ajali za barabarani,Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema serikali ina mkakati madhubuti ya kupambana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja kuongeza wigo wa elimu kwa njia ya redio ,luninga na machapisho ya vipeperushi.
Social Plugin