Klabu ya Azam FC imetangaza kuachana na Nyota wake 8 ambao inaelezwa kuwa mikataba yao imemalizika hivyo hawataongeza na kuanzia sasa ni wachezaji huru.
Afisa Habari wa Klabu hiyo Jaffar Idd Maganga amesema kuwa uongozi wa juu tayari umeshafanya mazungumzo na wachezaji hao na umewapa ruhusa ya kuangalia timu nyingine.
Maganga amewataja wachezaji hao kuwa ni nyota wa zamani wa Yanga Obrey chirwa, nyota wa zamani wa Simba Daniel Lyanga na Ramadhani Singano.
Wengine ni Joseph Kimwaga, Enock Atta, Tafadzwa Kutinyu, Steven Kingue na Hassan Mwasapili.
Wengine ni Joseph Kimwaga, Enock Atta, Tafadzwa Kutinyu, Steven Kingue na Hassan Mwasapili.
Maganga amesema kuwa Azam FC inawashukuru wachezaji hao, kwa mchango wao mkubwa walioutoa ndani ya Klabu hiyo na wana imani watafanya vizuri huko waendako.
Social Plugin