UONGOZI wa Azam FC chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin kwa kushirikiana na benchi la ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragaje umewaongezea mkataba wachezaji wake wawili leo ili waendelee kuitumikia timu hiyo msimu ujao.
Nyota hao wawili mikataba yao ilikuwa inamalizika ni pamoja na mlinda mlango Benedict Haule na kiungo Braison Raphael wote wameongeza kandarasi ya mwaka mmoja leo.
Azam FC wanatarajia kuingia kambini kesho kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kagame wakiwa wao ni mabingwa watetezi itakayofanyika nchini Rwanda mwezi Julai.
Social Plugin