Klabu ya Yanga imetangaza kuinasa saini ya Beki kiraka wa timu ya KMC, Ally Ally 'Mwarabu' ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.
Ally amekuwa mlinzi bora ndani ya Kikosi cha KMC kitu ambacho kilimvutia Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera na kuacha maagizo kwamba naye aongezwe kwa wachezaji wa ndani.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa mipango ya usajili inaendelea kwa sasa kwa wachezaji wa ndani kwani wale wa kigeni wamekamilisha maagizo ya mwalimu kwa asilimia 90.
Social Plugin