Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bunge Sports Club leo Juni 22,2019 wanatimuana Vumbi nene katika Bonanza la Michezo mbalimbali na timu ya wafanyakazi Benki ya NMB mchezo unaocharazwa kuanzia Majira ya saa 12:00 asubuhi.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika hafla fupi ya makabidhiano ya jezi za mchezo kutoka NMB Benki Kwenye Ukumbi wa Habari,Bunge, jijiniDodoma meneja wa timu Ya Bunge Sports Club ,Mbunge wa Ulyankulu Tabora Juma Peter Kadutu amesema amesema wamejiandaa kuwabamiza vyema NMB na kilichobaki ni kutimuliwa Vumbi tu kwani kila mwaka NMB Wamekuwa wakifungwa.
Kadutu ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tabora, na mjumbe wa TFF amesema wana uhakika wa kushinda kwa michezo yote ikiwa ni pamoja na mpira wa pete na watachukua kikombe.
Aidha,amesema wanajiandaa na michezo ya wabunge Afrika Mashariki ambayo hufanyika kila Mwaka huku mwaka huu ikitarajiwa kufanyika nchini Uganda huku pia akitumia fursa hiyo kuipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kusapoti kila Mwaka.
Mkaguzi wa ndani Benki ya NMB makao makuu Bw.Juma Kimori amesema Benki ipo sambamba na serikali katika kusaidia masuala ya kijamii.
Meneja wa NMB kanda ya kati ,Nsolo Mlozi amesema Benki hiyo imejikita kutoa huduma katika maeneo makuu manne katika kusaidia jamii ambayo ni sekta ya afya,Elimu,elimu Fedha na kuhudumia jamii katika majanga.
Aidha,amesema asilimia 1% ya mapato hurudi kuhudumia jamii ambapo asilimia 1% ya mwaka jana zilitengwa zaidi ya Tsh.Bilioni 1 na mpaka sasa zaidi ya Tsh.Milioni 450 zimetumika.
Michezo inayochezwa katika Bonaza hilo ni pamoja na Mpira wa miguu,mpira wa pete,mpira wa kikapu na Jogging.
Social Plugin