Mbunge wa Buyungu (CCM) Christopher Chiza amesema risiti za kielektroniki (EFDs) hasa zinazotolewa kwenye vituo vya mafuta hufutika baada ya muda na hivyo kuwafanya wafanyabiashara washindwe kutunza kumbukumbu.
Chiza alikuwa akichangia mapendekezo ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni bungeni jijini Dodoma jana Jumanne Juni 18, 2019.
Alisema Serikali inapendekeza kupunguza ushuru wa mashine za EFDs kutoka asilimia 10 hadi asilimia sifuri akisema ni jambo jema kwa sababu mashine hizo zinatumika katika kukusanya ushuru.
Alisema alihudhuria mkutano wa Chama cha wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo, (TCCIA) kwa ajili kufundisha jinsi mashine za EFDs zinavyoagizwa.
Chiza alisema walisema mashine hizo kama ilivyo kwa bidhaa nyingine wanaweza kucheza nazo hivyo wakati mwingine mashine hizo zinaweza zikawa hazitoi taarifa sahihi.
“Mashine nyingi hasa kwenye vituo vya mafuta ukiiweka nyumbani baada ya miezi mitatu minne hazisomeki tena yamefutika yote kama hujapiga picha basi hizo taarifa na kumbukumbu utakuwa hauna tena,” alisema.
Social Plugin