NA Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mpango Dokta Philiph Mpango wakati akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.
Dokta Mpango amesema kati ya kiasi hicho,deni la ndani lilikuwa Sh.trilioni 13.25 na deni la nje ni Sh.Trilioni 37.78 ambapo ongezeko la deni la Serikali linatokana na kupokelewa kwa mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa jingo la tatu la kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere,Ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa ,ujenzi wa miradi ya umeme ,ujenzi wa barabara na madaraja makubwa.
Aidha,Dokta Mpango amebainisha sambamba na ukopaji,Wizara imeendelea kufanya tathmini ya deni la Taifa kila mwaka ili kupima uhimilivu wake ambapo matokeo ya tathmini iliyofanyika Mwezi Disemba ,2018 inaonesha kuwa deni la Taifa ni himilivu katika kipindi cha Muda mfupi ,wa kati na Mrefu.
Hivyo,thamani ya sasa ya deni la Taifa[Present Value of Total Public Debt]kwa pato la Taifa ni asilimia 27.2% ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 70 na thamani ya sasa ya deni la nje kwa pato la taifa ni asilimia 22.2% ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55% huku thamani ya sasa ya deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 157.3% ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 240% na ulipaji wa deni la nje kwa kutumia mauzo ya bidhaa nje ni asilimia 15.2% ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 23%.
Hata hivyo,Dokta Mpango amesema ,serikali imeendelea kuhakikisha inalipa deni kwa wakati kwa kadri linavyoiva ambapo katika mwaka 2018/2019 ,serikali ilitenga kiasi cha Sh.trilioni 1.41 kwa ajili ya kulipa riba ya deni la ndani na hadi kufikia April,2019 Sh.trilioni 1.06 kimelipwa sawa na asilimia 75.18% ya lengo.
Pia,Serikali ilitenga sh.bilioni 689.67 kwa ajili ya kulipa riba ya deni la nje ambapo hadi kufikia April,2019 sh.bilioni 588.30 zimelipwa sawa na asilimia 85.30% ya lengo ,vilevile ilitenga Sh.Trilioni 1.66 kwa ajili ya kulipia mtaji wa deni la nje ,ambapo hadi kufikia ,April,2019 sh.Trilioni 1.23 zimelipwa sawa na asilimia 74.10 ya lengo na Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kusimamia deni la Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Mikopo ,dhamana na Misaada SURA 134 Pamoja na mkakati wa muda wa kati wa kusimamia madeni.
Social Plugin