Uongozi wa WCB pamoja na Wasafi Media kwa pamoja wamezindua rasmi Tamasha la Wasafi Festival 2019 ikiwa ni msimu mpya wa Mapinduzi ya Burudani nchini.
Msanii Diamond Platnumz ndiye ametangaza ujio wa Tamasha hilo ambalo litaanza July 7 mwaka huu, Muleba.
Wasafi Festival litafanyika sanjari na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya kondom ili kujikinga kupata virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini(VVU) na Ukimwi.
Tume ya Kupambana na Ukimwi Tanzania (Tacaids) itatoa elimu hiyo na ni mmoja wa wadhamini wa tamasha hilo. Mkurugenzi wa lebo ya WCB Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, kuna uwezekano mikoa ikaongezeka kwa kuzingatia mwamko wa washiriki kwenye mikoa minane ya kwanza.
Tamasha hilo litaanza Julai 12 wilayani Muleba mkoani Kagera, kisha litahamia Tabora Julai 14, na Iringa Julai 20.
“Tumejipanga kupeleka burudani ya kutosha kwenye mikoa husika na tutaendelea kutoa taarifa ya wasanii wangapi watashiriki na wangapi watatoka nje ya nchi,” amesema Diamond.
Social Plugin