Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Ikiwa leo Juni 23,2019 ambapo Tanzania imeungana na mataifa mengine Ulimwenguni kuadhimisha siku ya Wajane Duniani,Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii jinsia ,Wazee na Watoto Dokta.Faustine Ndugulile ametoa rai kwa jamii zenye ndoa za Asili kusajili Serikalini ili kuondoa usumbufu baadaye pindi wanapohitaji kutafuta haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na mirathi.
Dokta.Ndugulile ametoa rai hiyo leo Juni 23,2019 katika kilele cha siku ya Wajane Duniani ambapo kwa Tanzania yamefanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Dokta Ndugulile amesema hapa nchini Tanzania hususan vijijini watu wengi hawajui haki zao hivyo ni muhimu kusajili ndoa zao za asili katika mamlaka husika za serikali huku akizitaka Taasisi za serikali zinazohusika na masuala ya mirathi kutoa elimu kwa jamii kuhusu taratibu za Mirathi kwani pamekuwepo kwa baadhi ya ndugu wasio wahusika wamekuwa wakiwageuka walengwa wa mirathi na kujifanya wasimamizi wa miradhi kwa nia mbaya ya kujipatia mali huku walengwa wa Mirathi hiyo wakiachwa wakihangaika.
Katika hatua nyingine Dokta Ndugulile amesema maandalizi ya Wosia yanatakiwa kuanza mapema ili kuondoa na kupunguza migogoro ya mirathi inayojitokeza pindi mwenza mmoja anapofariki.
Hata hivyo,Dokta Ndugulile amewatia moyo Wajane na kusema kuwa Ujane sio Mwisho wa Maisha na kinachotakiwa ni kutokata tamaa bali ni kufanya kazi za maendeleo na kuinua uchumi kwao.
Siku Ya Wajane Duniani imekuja kutokana na kampeni za mwanasiasa mmoja Muingereza ambae, alifiwa na baba yake akiwa mtoto nchini India ambapo Serikali ya Gabon ilidhamini azimio hilo la Umoja wa Mataifa na Inakisiwa kuna takriban wajane millioni 245 duniani na 115millioni wanadhulumiwa wakikabiliwa na ukatili,umasikini na kutengwa na jamii.
Social Plugin