Maafisa wa polisi nchini Uganda wamemkamata jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 22 ambaye amekuwa akijifanya kuwa mwanamke kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.
John Mark Bukenya ambaye amekuwa akihudumu katika baa moja inayojiita Muhorro Rest House, alisema alichukua hatua hiyo kwa sababu ya kujitafutia riziki.
Mark alikamatwa baada ya mwenye klabu aliyokuwa akifanya kazi kuwaarifu maafisa wa polisi.
"Nilipomhoji kwa kina, jamaa huyo alikiri kuwa mwanaume, nilipigwa na butaa sana kwani alionekana kuwa mwanamke kabisa, kila siku angevalia rinda tofauti, mikufu, herini na hata viatu wa kike," Alisema mwenye baa.
Habari za kukamatwa kwa Mark zilithibitishwa na kamanda mkuu wa polisi wilaya ya Kagadi Romeo Onek Ojara ambaye pia alisema jamaa huyo alifanya hivyo kwa ajili ya kutafuta ajira.
" Tunamshikilia huku tukifanya uchunguzi, alikiri kuwa yeye ni mwanaume na anasema anapendelea kuchukuliwa kama mwanamke na kufanya mambo ya kike," Ojara alisema.
Social Plugin