Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Matemanga wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, Hekima Gregory maarufu Mvomela(49), amefariki baada ya kunywa pombe ya kienyeji aina ya gongo pasipo kupata chakula.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa ambapo amesema taarifa juu ya tukio hilo ilitolewa kwenye kituo cha Polisi cha Matemanga kutoka kwa Mratibu Elimu Kata ya Matemanga, Rashidi Nasoro.
Marwa mesema katika taarifa hiyo Nasoro alieleza kuwa Mwalimu Gregory alikutwa akiwa anakunywa pombe ya kienyeji aina ya gongo na inadaiwa kuwa alikuwa hajapata chakula na baada ya kumkuta katika hatua hiyo, hatua ya kwanza alipelekwa katika hospitali ya misheni ya Kiuma ambako alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu.
Alisisitiza kuwa katika historia yake inadaiwa kuwa inaonesha ilikuwa ni kawaida yake kunywa pombe kupita kiasi bila ya kupata chakula cha kutosha licha ya kuonywa mara kwa mara na viongozi wake.
Katika hatua nyingine watu watatu wakishikiliwa na Polisi kwa kukutwa na lita 3.5 za pombe hiyo.
Social Plugin