Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umeapa kujibu vikali shambulizi la kombora lililofanywa jana na wapiganaji wa Houthi nchini Yemen kwenye uwanja wa kiraia wa ndege kusini mwa Saudia na kuwajeruhi watu 23.
Muungano huo, wa waislamu wa madhehebu ya Suni ambao umekuwa ukipambana na vuguvugu la Kihouthi nchini Yemen linaloungwa mkono na Iran umesema shambulizi hilo la mapema jana lilidhihirisha kuwa Iran inatoa msaada kwa kile ulichokiita kuwa ni ugaidi wa nje ya mipaka.
Muungano huo ulisema kombora hilo lilipiga ukumbi wanakowasili abiria katika uwanja wa Abha, na kusababisha uharibifu.
Wahouthi walisema katika vyombo vyao vya habari kuwa walifyatua kombora hilo na kuupiga uwanja wa ndege wa Abha ulioko kusini mwa mpaka wa Yemen unaotumika kwa safari za ndani na za kikanda.
Social Plugin