Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar Mshibe Ali Bakari amewataka wahitimu watarajiwa wa kitivo cha sheria kutoka chuo kikuu cha Zanzibar University kuzingatia vyema waliyojifunza wakiwa darasani muda wote.
Aliyasema hayo jana wakati wa sherehe maalumu ya usiku wa sheria ilioandaliwa na kitivo hicho chini ya ufadhili ya kampuni ya inayojihusisha na sheria Stallion Attorneys.
Alisema ni lazima wanafuzi hao wafahamu kuwa elimu ya sheria inatokana na uwezo binafsi atakaokuwa nao mtu katika utendaji wake wa kazi.
Alisema bila ya kujituma katika elimu hio ya sheria hutaweza kufanikiwana na kuwataka wanafunzi hao kuongeza bidii zaidi kiutendaji watakapokua kazini.
Kutokana na mazingira hayo aliwashauri wanafunzi hao kuzingatia zaidi elimu ya kivitendo wakitambua kwamba Taifa linawategemea katika upatikanaji wa haki pindi watakapoanza kazi kwenye maeneo mbali mbali ndani na nje ya Tanzania.
‘’Leo hii mimi nina heshimika kila mahala ninapokwenda kwa sababu ya kuekeza vijana wengi kwenye taaluma hii ya sheria binafsi najivunia hili na nataka muwe kama nilivo mimi au zaidi yangu’’,aliongeza.
Aidha Jaji Mshbe alitoa wito kwa wanafunzi hao watakapomaliza masomo yao kutambua kuwa wanajibu mkubwa wa kuthamini wateja wao iwapo wataajiriwa kwenye kampuni au watajiajiri wenyewe kwa lengo la kuwatunza na kuwaenzi wateja wao.
Kwa upande wake mmoja miongoni mwa wamiliki wa kampuni Stallion Attorneys Shehzada Walii alisema katika fani ya sheria zipo changamoto nyingi lakini wahusika hawatakiwi kukata tamaa.
Alisema wapo baadhi ya wanafunzi wengi hushindwa kufikia malengo yao kutokana na kukata tamaa kufuatia changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Hata hivyo alisema uwepo wa changamoto hizo kwawanafunzi zikiwemo za ajira hawapaswi kurudi nyuma badala yake wanatakiwa kuongeza bidii zaidi katika kuonesha uwezo waliojifunza wakiwa darasani.
‘’Mimi binafsi wakati namaliza chuo kikuu ni mara kadhaa niliomba kujitolea sehemu mbali mbali nilikosa fursa lakini sikuwahi kukata tamaa nilihangaika kila leo ili nitimize ndoto zangu na hatimae leo hii kwa kiasi fulani nimefanikiwa’’aliongeza.
Aidha aiwataka wahitimu hao watarajiwa kufahamu kuwa hakuna safari rahisi katika kusaka mafanikio na kwamba wanalazimika kujituma zaidi sambamba na kuwa tayari kujitoa kwa ajili ya mafanikio yao.
Naye Mkuu wa kitivo cha sheria kutoka chuo kikuu cha Zanzibar University Dkt,Makame Mohamed alisema chuo hicho kitaendelea kuwajengea uwezo waanfunzi wanaosoma sheria kwa lengo la kuhakikisha wanauzika katika soko la ajira.
Alieleza kuwa kwa miaka mingi chuo chao kimekuwa kikitoa kozi hiyo ambayo anaamini ni bora zaidi na ndiyo maana wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya nje na ndani ya Tanzania hujiunga.
Social Plugin