TAARIFA KWA UMMA
WITO WA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA KUJITOLEA.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) anawatangazia Vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2019.
Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambapo muombaji anaishi.
Zoezi la kuchagua vijana linaanza mwezi Juni 2019. Vijana watakaochaguliwa wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliopangiwa mwezi Agosti 2019.
Aidha, kwa upande wa vijana wa Mujibu wa sheria, Jeshi la Kujenga Taifa limetoa orodha ya awamu ya pili ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita 2019 kwa ajili ya kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria.
Vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliopangiwa kuanzia tarehe 11 Juni 2019 hadi tarehe 16 Juni 2019.
Orodha kamili ya majina ya vijana wa mujibu wa sheria waliochaguliwa awamu pili na makambi ya JKT waliopangiwa na aina ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go tz.
Mkuu wa JKT anawaalika vijana wote waliopata fursa hiyo kuja kujifunza Uzalendo, Ukakamavu, Stadi za kazi, na stadi za maisha zitakazowasaidia kujiajiri mara baada ya kumaliza mafunzo hayo.
Sifa za Muombaji ni kama ifuatavyo-:
1. Awe raia wa Tanzania
2. Umri
a. Kwa kijana wenye elimu ya darasa la saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18.
b. Vijana wenye elimu ya kidato cha Nne umri usiwe zaidi ya miaka 20.
c. Vijana wenye elimu ya kidato cha sita umri usizidi miaka 22.
d. Vijana wenye elimu ya Stashahada umri usizidi miaka 25.
e. Wenye elimu ya Shahada umri usizidi mika 26.
f. Shahada ya uzamili umri usiwe zaidi ya miaka 30.
g. Vijana wenye elimu ya Shahada ya Uzamivu umri usizidi miaka 35.
3. Awe na afya njema,akili timamu na asiwe na alama yoyote ya mchoro mwilini (Tatto).
4. Mwenye tabia na nidhamu nzuri na hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.
5. Kwa vijana waliomaliza elimu ya Sekondari kidato cha Nne awe waliomaliza 2016,2017,2018 na wenye ufaulu ufuatao.
a. Wawe wamefaulu na wawe na alama(Points zisizopungua 32).
b. Kidato cha sita wawe na ufaulu daraja la kwanza hadi daraja la Nne.
6. Awe na elimu ya msingi aliyehitimu darasa la saba.
7. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa shule (Original Birth Certificate).
8. Awe na cheti halisi cha kumaliza shule (School Leaving).
9. Awe na cheti cha matokeo (Original Academic Certificate /Transcript.
10. Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi,Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM wala kuajiliwa na Idara nyingine Serikalini.
11. Asiwe amepitia JKT Operesheni za nyuma.
12. Asiwe amejiushisha na matumizi ya madawa ya kulevya bangi, na yanayofanana na hayo.
13. Kwa wale wenye Vipaji vya Michezo mbalimbali na Sanaa sifa za elimu nia sawa na zilizotajwa hapo juu.
JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:-
1. Bukta ya rangi ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic) iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu.
2. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
3. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
4. Soksi ndefu za rangi ya nyeusi.
5. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
6. Truck suit ya rangi ya kijani au blue.
7. Flana ya kijani kibichi yenye kola ya duara isiyo na maandishi.( dark green Tshirt with round colar).
8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
MAJINA YA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KWA AWAMU YA PILI YANAPATIKANA KWENYE MAJINA YA MAKAMBI YA JKT YALIYOPO HAPO CHINI.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 10 Juni 2019.
Social Plugin