Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI 11 ZA UTURUKI ZATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI


Ujumbe wa kampuni 11  kutoka Uturuki upo nchini kwa ajili ya kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji, hususan kwenye sekta ya viwanda vya dawa za binadamu, vifaa vya maabara, vyombo vya ndani,  vifaa vya umeme, ujenzi pamoja na ununuzi wa korosho.

Ziara hiyo imetokana na uratibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Ujumbe huo ambao uliwasili nchini tarehe 10 Juni 2019 ulishiriki mkutano (B2B) uliondaliwa na TPSF tarehe 11 Juni 2019. Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine,  wawakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Ukanda  wa Uwekezaji (EPZA) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) walitoa maelezo kuhusu kanuni, taratibu na mazingira ya kufanya biashara hapa nchini.

Ujumbe huo utatembelea Zanzibar tarehe 13 Juni 2019 na baadaye Dodoma kwa ajili ya kuangalia maonyesho ya masuala ya ujenzi. Ujumbe huo utaondoka nchini tarehe 16 Juni 2019 kurejea Uturuki.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com