DR. BASHIRU AHOJI MASWALI HAYA KWA WANAOSEMA UCHUMI WA TANZANIA HAUKUI

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Bashiru Ally amezindua ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano wa CCM mkoani Pwani,ambapo amechangisha zaidi ya milioni 25 na vifaa mbalimbali.


Katika uzinduzi huo, jumla ya mifuko ya saruji 2,861 imechangiwa ,nondo tani tano thamani ya milioni 9 ,malori ya mchanga, fedha taslimu ni sh.milioni 22.562 na ahadi ni sh.milioni 2.5 .

Alisema kati ya fedha hizo milioni tano imechangiwa na mwenyekiti wa CCM Taifa dk.John Magufuli.

Bashiru alisema, kwasasa hakuna mtindo wa kuchangia shughuli za kichama kwa fedha za mikononi ili kuweka mifumo mizuri ya kuaminiana.

Aidha alisisitiza ujenzi wa ofisi za chama ili kukijenga chama kwa maslahi ya wanaCCM.

“Uhai wetu unatokana na vikao na vikao haviwezi kufanyika chini ya miti,au kukutana gesti ,hivyo jengeni ofisi za chama kuanzia matawi na kata ili kuimarisha chama chetu”

Hata hivyo aliwasihi wananchi wasiwasikilize wale wanaokebehi Chama kilichopo madarakani na wale wanaopotosha kuhusu hali ya uchumi wa nchi.“Upotoshaji ni dhambi hasa kwa mtu aliyesoma chuo cha Dar es salaam na kusisitiza kwamba ,hali ya uchumi wetu ni imara” .

“Huwezi kudanganya watu na kuwaona ni wa pumbavu ,hakuna uchumi uliokufa ,hatuna deni la ndege,tunajenga vituo vya afya ,tunatundika nishati ya umeme hadi vijijini,watoto wanasoma bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne leo mtu unaibuka anasema uchumi umekufa”alikemea Bashiru.

Hakusita ,kuupongeza mkoa kwa kushirikiana ,kushikamana na kuwa na mahusiano mema baina ya serikali na chama. Aliweka wazi wilaya ambazo bado hazina mahusiano mazuri kati ya serikali na chama ikiwemo Bagamoyo ,Rufiji na Kibaha Vijiji ambako pale tatizo lipo kwa mkurugenzi mtendaji wa Kibaha Vijijini.

Alimjia juu mkurugenzi huyo wa wilaya ya Kibaha kwa kufanya kazi zake kwa mazoea na kushindwa kujenga mahusiano na ushirikiano na chama na kwenye majukumu yake ya kazi. Katika hatua nyingine akielekeza juu ya muelekeo wa chaguzi zijazo ,Bashiru aliwataka viongozi wanaokaa kwenye vikao vya maamuzi waache kutembea na wagombea mifukoni na badala yake waache wabunge,madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa waliopo wafanye kazi.

Pia aliwaasa baadhi ya wabunge kuacha kutumwa na kuwa wapiga debe kwa wawekezaji uchwara bali waelekezeni wawekezaji masharti na taratibu za nchi kwa maslahi mapana ya nchi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post