Serikali kupitia Wizara ya Madini chini ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imetoa toleo jipya la kitabu cha Madini yapatikanayo Tanzania kuanzia ngazi ya Mikoa, Wilaya na Kata.
Toleo hili la nne linaonesha taarifa nyingi zaidi ambapo maeneo mapya yenye madini yameongezeka zaidi ya 2200.
GST inatarajia kuwa kitabu hiki kitaongeza uelewa kwa wananchi na wadau mbalimbali kwa ujumla juu ya rasilimali madini yanayopatikana hapa nchini Tanzania na kuchochea uwekezaji katika sekta ya madini.GST inawakaribisha wadau wa sekta ya madini kujipatia nakala ya kitabu hicho kinachopatikana katika ofisi za GST jijini Dodoma.