Almaz
Derese (21), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari nchini Ethiopia amefanya mitihani (Kiingereza, Amharic na Hisabati) akiwa hospitali dakika 30 baada ya kujifungua, Juni 10 mwaka huu.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC), Almaz alitegemea kufanya mitihani yake kabla ya kujifungua, lakini iliahirishwa kutokana na mfungo wa Ramadhan.
Mwanafunzi huyo hakutaka kusubiri kufanya mitihani hiyo mwaka ujao, hivyo aliifanya nusu saa tu baada ya kujifungua.
Alisema kwa vile alikuwa anaitegemea mitihani hiyo, hilo halikuwa jambo gumu kwake, na mumewe, Tadese Tulu, alisema alikuwa amewaomba viongozi wa shule hiyo wamruhusu kufanya mitihani hiyo akiwa katika hospitali ya Karl Metu magharibi mwa nchi hiyo katika mkoa wa Oromia.
Nchini Ethiopia, ni kawaida wasichana kuacha shule na kurejea tena kuendelea, hivyo Almaz anategemea kufanya kozi ya miwili ili kujitayarisha kwa ajili ya kuingia chuo kikuu.
Social Plugin