MAAMUZI YA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA NEC YA CCM KILICHOONGOZWA NA MWENYEKITI RAIS MAGUFULI LEO

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na watanzania kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeketi leo Jijini Dar es Salaam chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ni mkutano wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Kikao pamoja na mambo mengine kimefanya uchaguzi wa kujaza nafasi moja iliyokuwa wazi ya Mjumbe wa Kamati Kuu na kuteua wanachama wa CCM wanao omba dhamana ya uongozi katika Chama, Jumuia na Serikali.

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) kwa kauli moja kimeazimia kuwapongeza Wanachama wa CCM na Viongozi kwa kazi nzuri ya kufuatilia utekelezaji wa ilani kote nchini Tanzania.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (HKT) wameazimia kwa kauli moja kupongeza Serikali za CCM za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) inayo ongozwa na Ndugu Rais John Pombe Joseph Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayo ongozwa na Ndugu Rais Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani na unaokwenda na wakati huku tukiwa tumepata mafanikio makubwa ya kuimarisha kiwango cha ukuaji wa uchumi wa asilimia 7.1 na 7.3 mtawalia ambao ni jumuishi.

Kwa kauli moja wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) wamewapongeza viongozi wawakilishi wa wananchi wanaotokana na CCM kwa kuendelea kuwa daraja kati ya wananchi na Serikali ya CCM ambayo wananchi wameichagua. Kikao cha HKT pia kimewapongeza Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wa CCM kwa kusimama kidete kujadili mipango na kupitisha bajeti za Serikali zenye mrengo wa kuwainua wananchi kutoka hali duni kwenda hali bora zaidi ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020.

Ikiwa ni sehemu ya kazi zake kikao cha HKT kimejadili na kupitisha kanuni za Chama Cha Mapinduzi katika maeneo ya;-

1.    Kanuni za Utumishi za wafanyakazi wa CCm na Jumuia zake Toleo la 2019
2.    Kanuni za Uteuzi wa Wagombea wa CCM katika vyombo vya Dola, Toleo la 2019
3.    Taratibu za Sehemu ya Wazee, Toleo la 2019
4.    Kanuni ya Jumuia ya Umoja wa Vijana wa CCM, kuhusu Idara na Uteuzi wa Wakuu wa Idara

Kikao cha HKT kimepokea na kuridhia kwa kauli moja pendekezo la Kamati Kuu la kumteua Ndg. Munde Tambwe kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT).

Halmashauri Kuu ya Taifa imewapendekeza ili wakashiriki katika uchaguzi katika ngazi husika wana CCM wanao omba dhamana za uongozi katika Chama na Jumuia kama ifuatavyo;-

Nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mkoa wa Kaskazini Pemba

Ndugu Omar Zubeir MBWANA
Ndugu Elizabeth Andrea MIHALE
Ndugu Abdulrahman Makame SHAKE

Nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mkoa wa Mkoa wa Kusini Unguja

Ndugu Makame Omar MAKAME
Ndugu Othman Ali MAULID
Ndugu Suleiman Ame VUAI (Kibeni)

Nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi, Mkoa wa Arusha

Ndugu Bakari Rahibu MSANGI
Ndugu Gerald Eliaika MUNISI
Ndugu Elipokea Wangael URIO

Nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi, Mkoa wa Arusha

Ndugu Fadhail Rajab MAGANYA
Ndugu Daud Ezron Daud MBISE
Ndugu Novai Megro MOLLEL

Nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Mkoa wa Arusha

Ndugu Selemani Qassim MSUYA
Ndugu Lovety PHILLEMON
Ndugu Omary Bahati LUMATO

Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Amani, Mkoa wa Mjini Unguja

Ndugu Juma Khamis HAJI
Ndugu Stumai Mohamed MSIMBE
Ndugu Faida Daud ABDALLA

Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Pangani, Mkoa wa Tanga

Ndugu Abdallah Ally ABDI
Ndugu Pili Ally OMAR
Ndugu Rajab Abrahaman ABDALLAH

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) kimepokea na kujadili taarifa ya Uhakiki wa Mali za Chama uliofanyika Zanzibar na kuelekeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuchukua hatua stahiki za kinidhamu kwa waliohusika na kupeleka mashauri yao kwa Kamati Ndogo ya Usalama, Maadili na Udhibiti wa Nidhamu kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kuhujumu mali za Chama.

Awali Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (HKT) imefanya uteuzi wa majina ya Wagombea wa nafasi za Umeya katika Manispaa za;-

Mtwara Mikindani, Mtwara
Ndugu Geofrey Isack MWANICHISYE

Ilala, Dar es Salaam
Ndugu Omary S. Kumbilamoto

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na,

HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post