Mahakama ya Afrika Mashariki imeanza kusikiliza kesi ya kupinga Sheria ya vyama vya siasa iliyofunguliwa na Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, Maalim Seif, Rungwe na Salum Mwalimu kwa niaba ya Vyama 8 vya upinzani Tanzania wakiiomba EACJ isimamishe matumizi ya sheria hiyo hadi kesi ya msingi itakapoamriwa.
Katika kesi hiyo ambayo viongozi wa upinzani wanawakilishwa na Mawakili Fatuma Karume, John Mallya na Jebra Kambole wanaomba mahakama kusitisha sheria hiyo.
Wakili Karume ameeleza majaji wa mahakama hiyo leo Jumatano Juni 19, 2019 kuwa sheria hiyo inakiuka mkataba wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika masuala ya haki na demokrasia.
Amesema miongoni mwa upungufu katika shauri hilo ni kuzuia viongozi wa upinzani kutoa elimu ya mpiga kura bila idhini ya msajili wa vyama vya siasa, kuzuia walinzi binafsi wa vyama na kuingiliwa uhuru wa vyama
Majaji wa mahakama hiyo bado wanasikiliza maombi ya upinzani kutaka mahakama hiyo kutoa uamuzi wa dharura kuzuia baadhi ya vifungu vya sheria hiyo.
Social Plugin