Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Juni 11, 2019 imetoka hati ya kumkamata mwigizaji , Wema Sepetu baada ya kukiuka masharti ya dhamana.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde baada ya mshtakiwa kushindwa kufika mahakama kusikiliza kesi inayomkabili.
Kabla ya kutoa uamuzi huo wakili wa Serikali, Silyia Mitanto amedia kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kusikiliza ushahidi lakini Wema na mdhamini wake wote hawakuwepo mahakamani.
Baada ya kueleza hayo, Ruben Simwanza ambaye ni wakili wa Wema amesema mteja wake alikuwepo katika mahakama hiyo lakini aliugua tumbo na kulazimika kuondoka.
Baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, hakimu Kasonde amesema, “Kama amekuja mahakamani halafu akaondoka bila kutoa taarifa, mahakama itajuaje kama alikuja? Alishindwa nini kutoa taarifa mahakamani.”
Baada ya kueleza hayo hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 4, 2019 huku akitoa hati hiyo ya Wema kukamatwa.
Social Plugin