MCHEZAJI TIMU YA TAIFA AONDOLEWA AFCON KWA KUONESHA MAKALIO

Kocha wa Algeria Djamel Belmadi amethibitisha kuwa amemtema kikosini kiungo mshambuliaji Haris Belkebla kwa utovu wa nidhamu.

Kikosi cha Algeria kinaendelea kujifua kwa ajili ya michuano ya Afcon, na kocha Belmadi amesema nidhamu ndiyo kipaumbele kwa sasa.

Mbadala wa Belkeba kwenye michuano hiyo itakayoanza Juni 21 ni mshambuliaji mzawa wa Ufaransa Andy Delort.

Tayari msahambuliaji huyo ameshatua kambini nchini Qatar.

"Kocha wa timu ya taifa Djamel Belmadi ameamua kumuengua kiungo Haris Belkebla kutoka kwenye kambi ya Afcon.

"Maamuzi ya kocha ni kwa ajili ya kudumisha nidhamu miongoni mwa wachezaji, kitu ambacho kwake ni kipaumbele," shirikisho la mpira la nchi hiyo limesema kwenye taarifa yake.

Hatua hiyo imefuatia picha ya video ya Belkebla inayomuonesha mchezaji huyo akionesha makalio yake kwenye mitandao wa kijamii.

Tukio hilo lilitokea wakati mchezaji mwenzake akiwa anacheza mbashara'gemu' kwenye mtandao wa kijamii.

Kiungo huyo wa klabu ya Brest tayari amaeshaomba msamaha akisema tukio hilo limemuacha akiwa "amevunjika moyo".

"Ningependa kuwaomba radhi. Hakika sikujua kwamba nilikuwa naonekana mbashara kwenye mtandao wa kijamii, hata hivyo, kile nilichokifanya kilikuwa nje ya maadili, na hakina nafasi kwenye mkusanyiko kama ule wa maana," ameandika kupitia mitandao yake ya kijamii.

"Si nia yangu kujitetea kwa makossa niliyofanya, na tayari ninayalipia kwa kuondolewa kwenye timu ya taifa.

"Nimevunjika moyo lakini ni adhabu halali kutoka kwa vyombo vinavyosimamia mpira vya Algeria. Hakika sina kinyongo kwa mtu yeyote isipokuwa nafsi yangu kwa kuwaangusha na kuwaumiza.

"Kwa unyenyekeu nawaomba msiihusishe familia yangu kwa kile kilichitokea, ambayo imenikuza kwa maadili mema kuliko kile nilichokifanya.

"Maadili yangu ni makubwa na yapo karibu kabisa na madili ya taifa letu. Kwa mashabiki wote, wafanyakazi wa timu, wachezaji, familia yangu na kocha

Belmadi, kikubwa ni kuwaomba radhi. Kwawachezaji wendangu, ndoto kwangu imeishia hapa, lakini natumai nitashangilia nanyi pale mtakaponyanyua kikombe. Idumu Algeria."
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post