Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PSSSF YATOA ZAWADI KWA KITUO CHA AFYA MAKOLE


Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, PSSSF, Bw. Paul Kijaizi (mwenye suti) akikabidhi zawadi kwa viongozi wa kituo cha afya Makole jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma Juni 21, 2019.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Mfuko Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi (aliyekaa kushoto), akiwa watumishi wengine wa Mfuko huo, wakimsikiliza mwanachama huyu (aliyekaa kulia), wakati alipotembelea ofisi za Mfuko jijini Dodoma. Katika Wiki hii ya Utumishi wa Umma, Mkurugenzi huyo wa Utawala aliungana na kitengo cha Huduma kwa wateja ili kuhudumia wanachama waliofika ofisini hapo kupatiwa huduma.
 Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Mfuko Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi (wapili kulia), akimsalimia mfanyakazi katika ofisi ya huduma kwa wateja PSSSF jijini Dodoma, ili kuungana nao kuhudumia wateja, wakati Taifa likiungana na nchi nyingine barani Afrika kuadhimishi Wiki ya Utumishi wa Umma Juni 21, 2019.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Mfuko akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya Dodoma.
***

Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma umetoa zawadi za ndoo za kuhifadhi kwa kituo cha Afya Makole, jijini Dodoma.

Akikabidhi zawadi hizo Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Mfuko Bw. Paul Kijazi alisema wameamua kutoa zawadi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma na ujirani uliopo kati ya PSSSF na kituo hicho cha afya.

“Kwa kweli nyinyi ni jirani zetu, mpo karibu nasi, lakini pia ujirani wenu ni maalum kwetu kwani baadhi ya watumishi na wapangaji katika jengo letu wamekuwa wakipatiwa huduma mbalimbali kwenye kituo chetu, asanteni sana”, alisema Mkurugenzi huyo.

Akipokea zawadi hizo, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Dkt. George Matiko alishukuru kwa msaada huo ambao alisema utaboresha usafi wa mazingira na kuwapunguzia hatari ya kukumbwa na magonjwa kwa wote wanaofika katika kituo hicho cha afya kilichofunguliwa mwaka 1980.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Mfuko Bw. Kijazi, ametembelea ofisi ya mkoa wa Dodoma na kukutana na wanachama wa Mfuko, pia alipata fursa ya kusalimiana na watumishi wa Mfuko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com