Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mama aliyejifungua watoto Mapacha wanne Radhia Solomon[24] mkazi wa Chemchemi Magomeni jijini Dar ES salaam na kutelekezwa na mmewe kwa madai ya kukwepa majukumu leo Juni 3,2019 amewasili bungeni jijini Dodoma ambapo bunge limeridhia kila mbunge wa kiume kumchangia Sh.Laki moja na kila mbunge wa kike kumchangia Sh.elfu hamsini fedha ambazo zitatumika kumsaidia kujikimu na kuwatunza watoto hao.
Akizungumza leo Juni,3,Bungeni jijini Dodoma Spika wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema jukumu la utunzaji wa watoto ni la kila jamii hivyo bunge limeamua kufanya mchango huo kwa wabunge ili kumsaidia mama na watoto huku akiwaasa wanaume kuacha tabia ya kutelekeza familia zao.
Ikumbukwe kuwa Radhia Solomon alijifungua watoto mapacha wanne Januari 8,2019 katika hospitali ya Muhimbili Dar Salaam ,watoto wa kike wawili Faudhia na Fardhia pamoja na wa kiume wawili Suleiman na Aiman ni pacha wanne ambao kila mmoja alikuwa na mfuko wake wa uzazi na gharama ya kuwanunulia maziwa ya SMA ya Kopo ni Sh.Elfu 40 kwa siku kwani alipojifungua afya yake haikuwa nzuri kunyonyesha hali iliyosababisha Mmewe kushindwa kumudu gharama na kuwatelekeza .