Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAREKANI YAKIRI NDEGE YAKE KUTUNGULIWA NA MAJESHI YA IRAN


Jeshi la Marekani limekiri Ndege yake kutunguliwa na jeshi la Iran ilipokuwa kwenye anga ya kimataifa kwenye eneo la mpaka kati ya ghuba ya Oman na Uajemi, maafisa wa Marekani wameeleza.

Awali vikosi vya kijeshi vya Iran vilidai kuwa vimeshambulia ndege ya kijasusi isiyo na rubani kwenye anga la Iran.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti tukio hilo dhidi ya ndege isiyo na rubani walioiita RQ-4 Global Hawk, kusini mwa jimbo la Hormozgan.

Jeshi la Marekani awali halikuthibitisha kama ndege yake imeangushwa, huku msemaji akikana taarifa kuwa ndege ya Marekani ilikua kwenye anga la Iran.

Tukio hilo limetokea siku kadhaa baada ya wizara ya ulinzi ya Marekani kusema kuwa watapeleka vikosi 1,000 zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati baada ya kutokea mvutano kati ya Marekani na Iran.

Marekani iliishutumu Iran kushambulia kwa mabomu meli za mafuta katika Ghuba ya Oman.

Mzozo huo ulishika kasi siku ya Jumatatu wakati Iran iliposema kuwa itazidisha kiwango cha urutubishaji wa madini ya Urani kinyume cha makubaliano na mataifa yenye nguvu duniani mwaka 2015.

Iran imefikia uamuzi huo baada ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com