Maafisa wa polisi eneo la Trans Mara Magharibi kaunti ya Narok nchini Kneya wamemkamata jamaa mwenye umri wa miaka 25 baada ya kupatikana na kosa la kumuua mwenzake aliyekisiwa kuwa mpenzi wa mkewe.
Mathew Langat aliripotiwa kumuua Stanley Bor kwa kumkata shingo baada ya kumfumania akishiriki ngono na mkewe wa miaka 22 nyumbani kwake majira ya saa nne usiku Jumamosi Juni 22.
Kisa hicho cha kushtua kimetokea katka kijiji cha Ng'endale, eneo bunge la Angata Barrikoi kule Trans Mara Magharibi.
Akithibitisha kisa hicho, chifu wa kata ya Angata Barrikoi Paul Kirui alisema mshukiwa alimvamia marehemu kwa mkuki na kumdunga shingoni na kwenye koo.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika mochuari ya hospitali ya Tenwek huku mshukiwa pamoja na mkewe wakitiwa mbaroni.
Chanzo - Tuko
Social Plugin