Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAKA AMUUA MDOGO WAKE AKIMHOJI 'KWANINI ANAPENDWA SANA NA BABA YAO'


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime /Rorya Henny Mwaibambe akionesh begi lililotumika kwenye wizi


Dinna Maningo, Tarime.

Mtoto mwenye umri wa miaka 7 Hassan Chacha ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kitagutiti Kijiji cha Getenga Kata ya Mbogi Wilayani Tarime ameuawa kwa kushambuliwa na kaka yake Mniko Chacha (20) kwa kumning'iniza  juu na kumtupa chini.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime /Rorya Henny Mwaibambe amesema  chanzo cha tukio hilo ni baada ya kaka wa marehemu kudai kuwa mdogo wake anapendwa na baba yao.

"Inasikitisha sana! kaka wa marehemu alimwambia marehemu kuwa kwanini wewe unapendwa sana,marehemu huyo ni mapacha Kurwa na Dotto, aliyefariki ni Dotto, ukiangalia umri wa watoto ni mdogo ni lazima wapendwe tu kaka yao ni mtu mzima hakupaswa kufanya huo ukatili",alisema Mwaibambe.

"Alimshambulia na kumning'iniza juu na kumtupa chini mara mbili akidai kwanini anapendelewa na baba yao kwa kuitwa mara kwa mara jikoni,marehemu alipata maumivu  ambapo alikimbizwa katika kituo cha Afya cha Dk. Steven na alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu"aliongeza.

Alieleza kuwa mtuhumiwa alitoroka baada ya kutenda tukio hilo na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea.

Wakati huo huo,Aliyekuwa mlinzi Kampuni ya POROMA aitwaye Fredy Nyangori (29) mkazi wa Mtaa wa Buhemba kata ya Bomani wilayani humo amekamatwa akiwa anataka kuiba kwenye duka la Voda Shop kwa kuingilia juu ya paa la chooni na kuvunja ambapo alikutwa akiwa na vifaa vya kuvunjia.

Mwaibambe alivitaja vifaa hivyo kuwa ni kamba kwa ajili ya kushukia,Bisibisi,Plies,Begi ambapo begi hilo ni la mlinzi mwenzake ambaye bado anafanya kazi kwenye kampuni hiyo na wote wamekamatwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com